Timu ya Yanga iliyokuwa imeshaongea na mchezaji Marcelin Koukpo na kufikia makubaliano ya kumsajili imegonga mwamba.
Imedaiwa kuwa Klabu ya mchezaji huyo ya huko kwao Benin Buffles du Borgou imekataa kumtema mchezaji huyo kwa kigezo kuwa huyo ni mchezaji tegemeo kwenye timu hiyo ya nyumbani na kwa sasa ipo katika harakati za kuwania ubingwa nchini humo