Kimenuka!!! HAJI MANARA AWASHUKIA VIKALI YANGA

Katika kile ambacho kinaonekana ni mwendelezo wa utani wa jadi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametupia kijembe kingine kwa wapinzani wao, Yanga.

Manara ambaye anajulikana kwa kuwa na utani mwingi hasa dhidi ya Yanga, ameweka picha inayoonekaa kuwadhihaki mashabiki wa Yanga ambao nao wamemcharukia kwa kumtolea maneno makali kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ofisa huyo amendika ujumbe huu: “Mwalimu Nyerere alitwambia 'kupanga ni kuchagua' ajabu ya baadhi ya wenzetu watatoa mapovu wakati wao wenyewe wamejichagulia!!!!koh koh koh!!!☺️😇”

Baada ya ujumbe huo Manara akaweka picha unayoiona kwenye ukurasa huu kuhusu mabosi wa klabu za soka.

Mmoja wa wachangiaji kwenye ukurasa huo anayejulikana kwa jina la Kassim Jumbe alisndika: “Sio lazma kupimwa akili hospital tu matendo yako na mdomo wako unatosha kuonyesha kuwa uyu mtu sio mzma ni hayo tu...

Mwingine aliyetambulika kwa jina la rafiki Donaina aliandika: “Shida sisi tunachoangalia ni mafanikio tu ya club yetu nyie dish liliyumba chombo kilikuwa kinazama baharin mkaona hapa sasa hatuna jinc ngoja tumpe timu mme wetu tu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.