YANGA: HABARI MPYA NA ZA MOTO MOTO KUTOKA KLABU YA YANGA

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, ameungana rasmi na wachezaji wa Yanga kwenye mazoezi yao baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa, Kilimanjaro Stars, ikiwa ni siku moja baada ya kutua nchini akitokea kwenye kikosi hicho.

Mshambuliaji Mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, Akiwa Mazoezini
Straika huyo ambaye tangu asajiliwe na Yanga hakuwahi kufanya mazoezi na kikosi hicho kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, jana kwa mara ya kwanza amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake huku akikutana uso kwa uso na washambuliaji wenzake kama Amissi Tambwe na kiungo Papy.
Kocha wa Yanga, George Lwandamina na Msaidizi Wake, Shadrack Nsajigwa, Wakiwaonyesha Mfano Wachezaji Wao

Yanga imeendelea na mazoezi ya uwanjani jana Uwanja wa Uhuru jijiniDar kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya FA na Ligi Kuu Barainayotarajiwa kuendelea karibuni.

Na Musa Mateja/GPL
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.