YANGA: HABARI MPYA KUTOKA KLABU YA YANGA LEO IJUMAA DISEMBA 29,2017

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga wako katika hatua za mwisho za kusaini mkataba mnono na kampuni ya vifaa ya Macron kutoka Italia.

Yanga ambayo ina mataji 27 ya Ligi Kuu kibindoni tayari imefanya mazungumzo ya awali na kampuni hiyo na huenda ikasaini mkataba huo mapema wiki ijayo

Macron tayari imesaini mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo watakuwa wakitoa vifaa kwa timu zote za Taifa. Macron pia itawapa TFF Sh400 milioni kila mwaka kwa miaka yote miwili ya mkataba.

Kulingana na Mwanaspoti, nyota wa zamani wa Yanga, Aaron Nyanda ndiye anayesimamia dili hilo. 

Nyanda ambaye ni Ofisa Masoko wa TFF, ndiye aliyekamilisha pia dili la Macron na shirikisho hilo.

Yanga inatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na Macron ambapo pamoja na mambo mengine, itapewa dola 250,000 (Sh556 milioni) kila mwaka.

Mbali na hivyo, Yanga itakuwa ikipokea mgawo wa faida kutokana na mauzo ya jezi zake kutoka kwenye kampuni hiyo, hivyo kila mwezi inaweza kuvuta kiasi kinachofikia Sh90 milioni.

“Dili linaweza kukamilika ndani ya siku tano ama sita zijazo. Dili lote linasimamiwa na Aaron Nyanda ambaye ndiye amefanikisha hao jamaa kusaini pale TFF, si unajua yupo kwenye Kamati ya Masoko ya Yanga, hivyo anawasaidia,” 

Yanga kwa sasa ina udhamini wa SportPesa inayoipa Sh950 milioni kwa msimu huu, Azam TV wanaowapa Sh272 milioni pamoja na Maji ya Afya ambao wanawapa maji ya bure mazoezini na katika mechi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.