Uongozi wa Simba umeongozwa na Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Haji Manara kufika nyumbani kwa kiungo wake, Mohamed Ibrahim ambaye alifiwa na mwanaye.
Manara aliongozana na wachezaji wa Simba kwa ajili ya kumliwaza mchezaji huyo ambaye alionekana mnyonge.
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma naye aliwaongoza wachezaji hao katika msafara huo.