YANGA: HABARI NJEMA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA YANGA

Straika mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, ameungana rasmi na wachezaji wa Yanga kwenye mazoezi yao baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa Taifa Stars ikiwa ni siku moja tu baada ya kutua nchini akitokea kwenye kikosi hicho.

Straika huyo ambaye tangu asajiliwe na Yanga hakuwahi kufanya mazoezi na kikosi hicho kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, leo kwa mara ya kwanza amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake huku akikutana uso kwa uso na washambuliaji wenzake kama Amissi Tambwe pamoja na Kiungo Papy Tshishimbi.

Yanga imeendelea na mazoezi ya uwanjani leo, yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, kwa ajili ya maandalizi ya michuano ile ya FA pamoja na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea hivi karibuni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.