Klabu Bingwa nchini Tanzania na Mabingwa wa zamani wa Afrika Mashariki klabu ya Yanga kwa staili yao ileile ya Kimya Kimya katika masuala ya usajili inadaiwa tayari imeingia katika harakati ya kunasa saini ya Mkenya Ochieng Ovella.
Ochieng Ovella alionekana kusumbua vilivyo ngome ya Kilimanjaro Stars hasa upande wa Kushoto kwa Gadiel Michael kuna taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Yanga kuwa kamati ya Usajili ya klabu ya Yanga chini ya Mnyika imekaa ili kuangalia namna ambavyo inaweza kudaka haraka saini ya winga huyo.
Mchezaji huyo alionekana kucheza kwa kasi na kuwa mjanja mjanja kiasi cha kuonekana mabeki wa Stars kushindwa kumkaba kiungwana na Kuanza kumchezea Rafu, Ochieng anayecheza katika klabu ya Kariobange bado anamkataba wa mwaka mmoja Na Timu yake lakini Yanga wameonekana kuvutiwa sana na kiwango chake wakiamini anaweza kuwa mrithi sahihi wa Msuva.
Katika mchezo kati ya Harambee Stars na Kilimanjaro Stars Ochieng Ovella ndiye aliyekuwa mchezaji Bora wa mchezo Huo.
Yanga wanahaha kuimarisha kikosi chao ili kufanya vizuri michuano ya kimataifa na kutetea Ubingwa wao ambapo wakiuchukua msimu huu itakuwa mara ya nne mfululizo kwa Yanga kufanya hivyo