TSHISHIMBI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MICHUANO YA KIMATAIFA BARANI AFRIKA

TSHISHIMBI afunguka na kwaiambia juu ya, Simba na Yanga pamoja na kupangiwa vibonde kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika, lakini pia watakuwa na kibarua kizito cha kumaliza mchezo mapema kutokana na kupewa nafasi ya kuanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ambao wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wao wamepangwa na St. Louis ya Shelisheli, huku wenzao Simba wakipewa Gendarmerie Tnale ya Djibout.

Katika hafla ya droo hiyo iliyofanyika jana jijini Cairo yaliko Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Yanga watajitupa uwanjani Februari 9 au11 mwakani kuvaana na St. Louis iliyoanzishwa mwaka 2007 na kufanikiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mara tano, Kombe la Washindi mara mbili na Kombe la Shirikisho mara moja, lakini haijawahi kuvuka raundi ya kwanza katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Hivyo, Yanga wakifanikiwa kuitoa timu hiyo, wanaweza kukutana na El Merrikh ya Sudan ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuiondoa Township Rollers ya Botswana.

Nao Simba watacheza mechi yao ya kwanza ya shirikisho dhidi ya Gendarmerie Tnale katika tarehe ambazo Yanga watacheza, hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndio litajua namna ya kupanga; kama Yanga watacheza Februari 9 mwakani basi Wekundu hao wa Msimbazi watacheza kesho yake.

Kama Simba watafanikiwa kuichapa Gendarmerie, watakutana na mshindi kati ya wakali wa Ligi Kuu Misri, El Masry au Green Buf­aloes ya Zambia, huku mabingwa wa Zanzibar, JKU ambao watakuwa na Yanga kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wao watakutana na kimbembe baada ya kupangiwa kuvaana na Zesco ya Zambia.

Zesco mwaka jana waliinyofoa Yanga kwenye michuano hiyo, hivyo bila shaka JKU watakuwa wanajua kazi watakayokutana nayo dhidi ya miamba hiyo ya Zambia na kama wakifanikiwa kuvuka hatua hiyo, bado watakuwa na kazi kubwa mbele ya Asec Mimosas ya Ivory Coast na Benin.

Nao Zimamoto itakayoambatana na Simba kulifukuzia Kombe la Shirikisho, itakutana na Wolaitta Dicha ya Ethiopia, wakati kikosi hicho cha Zanzibar kimeshiriki mara moja wapinzani wao ndio wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Zimamoto wakifanikiwa kuwang’oa Wahabeshi hao, watavaana na Zamalek ambayo mwaka jana ilifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.