HABARI 2 MPYA KUTOKA KLABU YA YANGA ZILIZOTUFIKIA ASUBUHI HII 3/02/2018

Wakati watu wakiwa wamekata tamaa kabisa juu ya Urejeo wa Mchezaji Donald Ngoma ndani ya Kikosi cha Yanga kutokana na kuwa majeruhi wa Muda mrefu ndani ya Klabu hiyo ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Daktari ameelezea kidogo Kuhusu Afya ya Mchezaji huyo

Dr Bavu amesema Donald Ngoma atarejea kwenye mazoezi na wenzake mara baada ya Kumaliza program Maalumu ya Gym ambayo yupo chini ya Madaktari wanaomfatilia maendeleo Yake

Akimaliza Mazoezi hayo maalumu ndipo ataungana na wenzake kwa mazoezi ya pamoja, Ngoma alianza kwa kuumwa nyama za Mapaja, Kabla ya Kuja kuumia Goti na Kisha wakati akielekea Kuwa Fiti akaumia Kisigino akiwa anaendelea na Program ya Gym

LIPULI VS YANGA, LIPULI KUFURAHIA KUKOSEKANA KWAKE

Yanga leo wanacheza mchezo dhidi ya Lipuli lakini moja kati ya Vitu watakavyomiss ni huduma ya Mchezaji huyo ambaye katika mchezo wa kwanza jijini Dar Es Salaam ndiye aliyefunga bao la Kusawazisha akifunga bao kwa Kichwa na Kusawazisha bao ambapo lipuli walitangulia kuwafunga Yanga mapema kupitia kwa Abdallah SEIF KARIHE

Lipuli wanafurahia Kukosekana kwa Ngoma kwakuwa ndiye aliyewatibulia Ushindi wao siku hiyo katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam


Credit- kwataunit
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.