HABARI MPYA ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA SIMBA ASUBUHI YA LEO 3/02/2018

Kama ulifikiri Simba wamekaa kaa tu kizembe kuelekea michuano ya Kimataifa basi hiyo Futa kabisa kichwani kwani mipango muda ishapangwa na kuandaliwa kuhakikisha WaDjibout wanakufa kwa bao za Kutosha tu kipindi watakapokutana na Simba katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba kumbe toka December mwaka jana ilimtuma mmoja ya wajumbe wa kamati ya Mashindano huko Djibouti kuwafatilia wapinzani wao Gendarmeria Tnale;ili kuwajua vyema kuanzia Mbinu wanazotumia, Nguvu na udhaifu wa timu hiyo INpokuwa uwanjani na mambo mengine mengi ya Kitaalamu.

Mara baada ya Simba kumtuma kigogo huyo alifanikiwa kuwaona Live uwanjani Gendarmeria Tnale wakicheza katika mchezo wao wa Ligi dhidi ya timu ya PORT ukiwa ndiyo mchezo wa mwisho wa Ligi ya Djibouti.

Ukiachana na kuwaona Live Simba pia wamefanikiwa pia Kupata CD za mechi ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza na timu mbalimbali.

Mara baada ya kamati ya Mashindano kukamilisha kazi ya kukusanya data za Wapinzani wao kamati iliwasilisha kwenye benchi la Ufundi la Klabu ya Simba ili kufanyia kazi.

Kocha mkuu wa Simba Pierre Lechantre amesema kwasasa hawezi kuongelea mchezo huo bali akili yake ipo kwenye mchezo wa Ligi Kuu VPL mchezo kati ya Simba na Ruvu Shooting Jumapili
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.