Mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili unatatajia kupigwa kesho Jumamosi katika Uwanja wa kumbukumbu ya Samora.
Mchezo huo umeileta Yanga mkoani Iringa na katika uwanja huo baada ya miaka 16.
Timu hiyo iliingia katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Elimu kishiriki cha Mkwawa kwa ajili ya kufanya mazoezi. Timu hiyo ilifanya mazoezi kwa muda wa saa moja.
Umati wa watu ulifurika katika uwanja huo kufuatilia mazoezi ya timu hiyo yenye makao makuu mitaa ya Twiga na Jangwani.