RUVU SHOOTING YATAJA TEKNOLOJIA ITAKAYOTUMIKA KUWAUA SIMBA MECHI YA JUMAPILI

Kuelekea kwenye mchezo wa ligi kati ya Ruvu Shooting vs Simba Sc, ambao ni mchezo wa kwanza katika mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania msimu wa 2017-2018.

Afisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire ametamba kuifunga Simba Sc kwa kutumia Teknoloji ya Kienyeji.

Masau alisema kuwa kipigo cha goli 7 walichokipata mwanzoni mwa msimu huu dhidi ya Simba ilikuwa ni bahati tu waliyopewa na Mungu.

Kuelekea kwenye mchezo huo Msau Bwire amesema Ruvu Shooting wana mfumo mpya watakaoutumia nao unaitwa Kupapasa.

"Tuna teknorojia ya kienyeji kwa mfano unapokwenda maeneo yanayoitaji ukaguzi, kuna vyombo vya kisasa vinavyotumika kukagulia mfano (Airport) utapita kwenye mashine kama una kitu kibaya alamu zitalia utapitisha vifaa vyako kwenye kwenye mashine wataangalia kwenye Computer kama kuna kiti kimejificha huko kitaoneka".

"Lakini kama hawajalidhika na ukaguzi wa mashine zao (hupapasa) kwa mikoni hii ni teknorojia ya kienyiji ninayoisema sasa sisi tuna plan na tunapanga kuwapapasa Simba Jumapili hii".

Masau Bwire aliongeza kuwa klabu yake iko vizuri mno, imefanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanamfunga Simba.

Klabu hiyo ilitolewa katika mashindano ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) au FA juzi baada ya kufungwa na Majimaji ya Songea katika uwanja wa Majimaji, Songea goli 2-1!

Baada ya kutolewa Masau alisema kuwa mpira, ndivyo ulivyo, utacheza lakini kama si riziki, utaliwa tu hata na Kibogoyo! Jana(Juzi) pamoja na ugumu wote ule, Kibogoyo katutafuna!.

Mwanaume kamili akipigwa anajipanga kupiga kama si aliyempiga basi, atapiga wa mbele yake.

Mbele yetu yupo yule wa pale Kariakoo, ni mkali kwa sasa lakini tumejizatiti kumpiga.

Tutampiga kistaarabu sana, teknolojia ya juu sana katika kumpiga itatumika, amini tutampiga, tutampiga kisayansi, teknoloji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.