watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeanza kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuanza kuifutalia St Louis kimyakimya.
Mmoja wa viongozi wa Yanga aliweka bayana kwamba tayari wameanza kuifuatilia timu ambayo watakutana nayo mwezi ujao. Alisema maandalizi yao ya awali ni pamoja na kuwafahamu vyema wapinzani wao.
Kikosi hicho cha Jangwani kinatarajiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wao na St Louis mwezi ujao Februari 27, mechi ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar esa Salaam.
Miongoni mwa mambo ya muhimu ambayo benchi la ufunfi linayaanya kuelekea mchezo huo ni pamoja na kutaka kufahamu mbinu za wapinzani wao na aina ya mpira wanaocheza.
Pia lengo la kuanza maandalizi hayo ya awali ni kutaka kujua hoteli ambayo watafikia ili kupekupa kufanywa fitina za nje ya uwanja.
mwanaspoti