Beki mahiri wa Simba, Asante Kwasi amejikuta akipajikwa majina sawa na idadi ya makabila 120 yanayokadiriwa kuwepo hapa nchini, yanayotumia lugha za Kibantu.
Jina la ‘Asante’ ndiyo limenyumbulishwa na kutafsiriwa kwa lugha za makabila ambayo kila kabila linaita neno neon hilo kwa matamshi yake.
Mashabiki mtandaoni waliandika majina mbalimbali yanayomaanisha neno asante kwa makabila yao huku wakimalizia na jina la ubini la Kwasi.
Kwa mfano kabila lako neno ‘asante’ jinsi linavyoanza unamalizia na neno Kwasi, jambo ambalo limeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii, lakini hayo yote ni mwendelezo wa mashabiki wa Simba kusherehekea ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Singida United jana Alhamisi.
Mabao ya Simba yalifungwa na Shiza Kichuya, Asante Kwasi na Emmanuel Okwi akiweka mabao 2.
mwanaspoti