Leo ni siku ya kwanza kikosi cha Simba kimeendelea ikiwa ni baada ya kujua itacheza na nani katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Simba imepangwa kuanza na Gendamarie ya Djibouti ambayo si timu ngumu sana ingawa haitakiwi kudhauliwa.
Simba imeendelea kujifua kujiandaa na Ligi Kuu Bara katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jeshi la Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Simba imekuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja huo kuhakikisha kikosi chake kinakaa vizuri.
Kwa takribani wiki moja, kikosi cha Simba kipo chini ya Kocha Msaidizi Madoud Djuma raia wa Rwanda.
Kocha huyo amekuwa akitoa mazoezi mbalimbali na zaidi ni yake ya kutaka wachezaji kuwa na wepesi pia ya ufundi katika ufungaji na kuzua kulingana na hali halisi.